About Us

Get to know MLVTC

Elmeleck Kigembe, Katibu Mkuu wa KKKT - Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ”Ninakipenda chuo cha MLVTC. Katika mkoa wetu, kwa vijana wenye hamu ya kujiendeleza kimekuwa chuo cha kuwafanya waendane na enzi hii ya viwango vya kidijitali visivyoweza kuzuilika.”
Goldian Nteboya, Mkuu wa Chuo: “MLVTC ni ufunguo wa maisha ya kisasa kwa vijana.”
Nicolaus Tinkamwesigile, Naibu Katibu Mkuu wa KKKT - Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ”MLVTC imekuwa suluhisho kwa ajira ya vijana.”
Mchg. Frederick Muganyizi, Mchungaji wa Jimbo la Kusini B; KKKT-DKMG “MLVTC: Taasisi ambayo kwayo kijana anapata stadi za maisha kwa kumfungua macho katika soko la enzi ya kidijitali ambamo fursa hazitegemei tu kuajiriwa.”
In my job in State administration of Agriculure I learnt that a sound vocational training is a very good base to earn one's living. And it helps a lot to face all challenges of new developments upcoming. So I am glad I can support Muleba Lutheran Vocational Center.
Juergen Nachtigal: “Katika wajibu wangu kama Bwana Utawala wa Kilimo Kitaifa nilijifunza kwamba msingi mzuri wa kujipatia kipato kizuri maishani ni wa kupata mafunzo ya ufundi. Elimu hii husaidia kukabiliana na changamoto mpya zinazojitokeza kimaendeleo. Kwa sababu hiyo ninafurahi na kutosheka katika kuwezesha MLVTC.”
Klaus Klurse: “ Tangu nilipofika Tanzania kwa mara ya kwanza nilianza kuwekeza nguvu na bidii nyingi kuhakikisha kwamba MLVTC panakuwa mahali pa kupata elimu bora na mazingira rafiki ya kujifunzia na baadae kupata ajira nzuri.”

Historia ya MLVTC

MLVTC ilianzishwa kama Taasisi binafsi ya uhisani katika udugu kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Magharibi (KKKT/DKMG) na chama cha uhisani kwa wahitaji kiitwacho Chama cha Elimu Ufundi Stadi Tanzania (Berufsbildung Tanzania e.V BBT) mwaka 2012. KKKT/DKMG na BBT ndiyo wamiliki wa MLVTC.

BBT is a small group of private persons of different religions who aim to support the vocational training of young people in Tanzania. The main purpose of BBT is to raise the funds needed to finance investment and equipment for the MLVTC, as well as student scholarships.

MLVTC inafanya kazi chini ya Bodi ya utawala ambayo wajumbe wake ni:

  • -Goldian Nteboya (Mkuu wa Chuo)
  • -Nicolaus Tinkamwesigile (Meneja), (part time Manager)

DHAMIRA

MLVTC kutoa elimu ya ufundi yenye kiwango bora ikiwa na usajiri wa VETA kuelekea kushinda mitihani na kupata cheti cha VETA ngazi ya II.

The Supervisory Board  gives advice to the Management and supervises the work of the MLVTC Management.

Wajumbe wa Bodi ya usimamizi wa chuo:

  • -Bw Klaus Luerse, Mwenyekiti, mjumbe kutokea BBT (klurse@klurse.de) -Mchg Elmereck Kigembe, Mwenyekiti mwenza, Katibu Mkuu KKKT/DKMG -Mchg Frederick Muganyizi, Mchg wa Jimbo Kusini B, KKKT/DKMG -Bw Nicolaus Tinkamwesigile, Meneja wa muda -Bw Juergen Nachtigal, mjumbe kutokea BBT
    • mail: klurse@klurse.de
  • Rev. Elimelech Kigembe (Co-Chairman, General Secretary ELCT-NWD)
  • Mchg. Frederick Muganyizi (Jimbo Kusini B) KKKT/ DKMG
  • Jürgen Nachtigal (Mjumbe kutoka BBT)

Madhumuni

1. Kuwaelimisha vijana kutoka vijijini na mijini katika fani mbalimbali kwa muda maalumu. 2. Kuwawezesha vijana kujipatia kipato kwa kuajiriwa au kujiajiri. 3. Kuwaajiri na kuwawezesha walimu bora ili waweze kufundisha kwa kufuata madai ya muhitasari kwa mtaala. 4. Kujenga uongozi bora kiutawala ili kuendesha chuo kuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia na kujiendeleza.

Kutana na walimu wetu

Walimu hawa watakuwa nawe na kukuongoza katika safari yako ya kujifunza hadi wakati wako wa kuhitimu masomo.

Jackline Vedasto

Mratibu wa Mafunzo na Matron

Shahada ya kwanza ya Sayansi (Bachelor of Science)

 

Josiah Dominic

Trainer: Computer Mathematics, ICT            

Degree: Bachelor of Science (ICT)

 

David Ezekiel

Afisa Msaidizi na Mkufunzi wa TEHAMU/Fundi sanifu

Degree: VETA-Level II in ICT

Aidath Saad Amri

   ICT Trainer/  Short courses

Degree: VETA-Level II in ICT

Denis Rutta

Electrical Installation Trainer

Degree: VETA-Level III in Electrical Installations

swSwahili