MLVTC
Muleba Lutheran Vocational Training Centre

Karibu unufaike na elimu ya ustadi wa maisha kwa ajira nzuri.

Elimu kwa Vitendo

MLVTC ni chuo chenye namba ya usajiri VET/KGR/FR/2020/C 72 Mhitimu wa kozi ndefu hupata cheti cha VETA ngazi ya II

Kozi za kipekee

1. Information and Communication Technology (ICT)
2. Electrical Installation (EI)

Vifaa vya kisasa

- Computer laboratory with PC for each student
- electrical workshop
- well-equipped dormitories

MLVTC – Mahali pa mafunzo bora kimatendo

Benetson Kamugisha, Principal of MLVTC

MLVTC offers Training in ICT and Electrical Installation. Both Fields in today’s digital age have become essential for success in many areas of life. In this modern world, Humans depend on them to facilitate all operations and activities. These skills improve the standard of living and create opportunities for everyone. They have made our lives easier, more effective and more productive. If you want to acquire computer or Electrical installation skills, MLVTC is the right place for you.

Walimu mahiri

Walimu wetu mahiri hutumia nguvu zao kuwasaidia wanafunzi katika kujifunza kwao. Tunapigania wanafunzi wenye juhudi na bidii katika kujifunza.

Wanafunzi wenye bidii

“Mchumia juani hulia kivulini” NA "Mtaka cha uvunguni sharti ainame". Juhudi na nidhamu katika kujifunza ni msingi mkubwa wa mafanikio ya mitihani na baadaye ajira nzuri. Huo ndio mchango wa wanafunzi wetu kwa mafanikio yao.

Miundombinu

Tangu mwanzo chuo hiki kimekuwa kikipata msaada kutoka kwa marafiki zao huko Ujerumani. Msaada huo umewasaidia kujenga madarasa mazuri, mabweni safi, jiko zuri na bwalo linalofaa. Aidha msaada huo uliwezesha kupata samani, mahabara ya kompyuta na karakana ya umeme vyote vikiwa na zana na vifaa vya kisasa.

MLVTC katika namba

1

       wanafunzi

1
Walimu
1
Kozi zitolewazo
1
Majengo chuoni kwetu

Jisikie kuhitaji kupata mafunzo yetu ya ufundi stadi

Nakuhakikishia kwamba hakuna njia ya kupata ajira ya kukuingizia kipato kizuri mbali na kupata mafunzo katika chuo MLVTC.

Klaus Lurse na Bernhard Troja, waasisi wa MLVTC

Sisi waasisi wa MLVTC na marafiki wa Ujerumani tunajitahidi kuchanga fedha ili kuweka mazingira rafiki ya upatikanaji wa vifaa vya kisasa na mafunzo stadi chuoni MLVTC yaani:-

Wadau wenye uwezo (kampuni kubwa, taasisi za mafunzo na serikali ya Ujerumani hutoa kompyuta zilizokwisha tumika (zinazofaa) na zana nyingine ambazo hutumika katika mafunzo chuoni MLVTC.

Vijana wa kujitolea na wataalamu wastaafu kutoka Ujerumani huwasaidia walimu wetu chuoni kuendeleza mafunzo ili kuwapa wanafunzi wetu fursa ya kuzungumza Kiingereza na kufahamu mwenendo na tabia za kazi za nchi nyingine.

Wayasemayo wanafunzi wetu

Nilipata elimu ya TEHAMA hapo MLVTC miaka 2017 na 2018 na kupata cheti cha VETA ngazi ya II. Maarifa niliyoyapa yaliniwezesha kupata kazi ya ukusanyaji data/takwimu hapo NGO ya Dimaye. Kwa kuwa mshahara wangu unaridhisha ninaweza kupata mahitaji yangu muhimu bila shida. Mwajiri wangu hunilipia makato yangu ya kijamii (NSSF) yatakayonifaa uzeeni. Nilitumia muda wangu vizuri wa kujifunza nilipokuwa chuoni MLVTC. Nilifurahia ushirikiano nilioupata kutoka kwa walimu wangu na wanachuo wenzangu. Tulijisikia huru kuomba msaada wa kimafunzo kutoka kwa walimu wetu waliokuwa wakarimu. Lilikuwa jambo la kushukuru sana kwamba kila mwanachuo alipata kompyuta yake binafsi kutoka chuoni MLVTC. Hilo laonesha jinsi mazingira ya kujifunza yalivyo rafiki hapo MLVTC.
Maisha ya mafunzo hapo MLVTC yalikuwa mazuri na ya kufaa kujifunza. Nilipenda kazi zote hapo chuoni zilizotushughulisha kikamilifu darasani na bustanini. Kwa sasa nimeanzisha mradi wangu mdogo wa kufundisha kompyuta na kazi nyingine zinazohusiana na maarifa ya kompyuta. Hapa ninawasaidia wenzangu na majirani kudizaini vitambulisho vya aina mbalibali za bidhaa na mabango. Haya nisingeweza kuyafanya kama nisingepata maarifa hayo hapo MLVTC. Kwayo ninajipatia kipato na kupata mahitaji yangu kimaisha.
Nilijiunga kusoma kozi ndefu ya TEHAMA hapo MLVTC miaka 2017-2018 nikahitimu kwa kupata cheti cha VETA ngazi ya II. Maarifa niliyoyapata yalinisaidia kupata kazi ya ukarani. Sina mshahara mkubwa ila kwa huo ninaweza kupata mhitaji yangu. Hata hivyo ninategemea kupata nyongeza ya mshahara. Maisha ya chuo yalikuwa mazuri kwangu hata nikaweza kuchaguliwa kuwa Rais wa wanachuo. Walimu walifundisha kwa budii na wanafunzi tulikuwa na mahali pazuri pa kulala na chakula kizuri. Ninawashawishi watu wengine kujiunga MLVTC kwa kuwa huko mtu atapata elimu nzuri, stadi za maisha na kujua hatua nzuri za kujifunza.
swSwahili