Ufadhili wa masomo

Marafiki zetu wa Ujerumani wa Berufsbildung Tanzania e. V. (BBT) wamelenga kutoa ufadhili wa masomo kwa baadhi ya wanafunzi wenye familia zisizokuwa na uwezo wa kulipa ada za chuo.

Dhima ya BBT

Waliposaidia kuanzishwa kwa MLVTC, nia ya BBT ilikuwa kupambana dhidi ya umaskini. Kwa kuwapa vijana fursa ya kupata mafunzo na stadi za By offering young people the chance to receive training in skills and abilities which will enable them to find well-paid work after graduation, they lay the groundwork for self-support and a life without help from outside. Waliposaidia katika kuanzishwa kwa MLVTC, fikra kuu ya BBT ilikuwa kupambana na umasikini. 

Kwa kuzingatia hayo, BBT inataka kuhakikisha kuwa hata vijana watokao katika familia masikini wanapata fursa ya kusoma MLVTC. 

Licha ya rasilimali chache BBT inaweza kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wachache kila mwaka.

 

Vigezo

  • Umefaulu elimu ya kidato cha nne. 
  •  Kiongozi wa kidini katika jamii yako athibitushe kuwa familia yako haina uwezo wa kuweza kulipa ada.
  •  Uwe menye nidhamu na matokeo mazuri chuoni.
  •  Umesajiliwa kwa masomo ya kozi ndefu chuonni kwetu.

Namna ya kuomba ufadhili wa masomo

  • Andika barua ya maombi ya ufadhili kwa kusaidiwa na Mkuu wa Chuo au walimu wa MLVTC kwenda kwa BBT.
  • Ambatanisha barua ya kiongozi wako wa kidini.
  •  BBT itapitia maombi yako na itathibitisha ufadhili wako iwapo utakuwa umefanikiwa.
  •  BBT inaweza kusitisha ufadhili wa masomo yako iwapo utakuwa mtovu wa nidhamu au kuwa na mwenendo hafifu wa kitaaluma.
swSwahili