HUDUMA ZETU

MLVTC ni zaidi ya chuo!

MLVTC hutoa huduma za kuaminika

 MLVTC kina nia ya kuwa kitovu cha ubora katika kuunda ujuzi na umahiri unaohitajika kitaaluma na kwa ajili ya ajira. Hii haihitaji tu mafunzo mazuri katika nadharia ya somo (darasani) bali uzoefu pia wa kufanya kazi halisi. 

Kwa sababu hii chuo kinatoa huduma zake kwa wanajamii pia. Tunatoa kazi za viwango vya juu. Kazi hizo kwa ajili ya wateja husimamiwa na walimu wetu wazoefu na kwa hufanyika kwa bei nzuri.

MLVTC ni shirika la hisani! Tunaahidi kwamba mapato yetu yote kutokana na ada na huduma kwa wateja yatatumika kuboresha kituo cha mafunzo!

Huduma za Kompyuta (TEHEAMA)

Kompyuta yako ina hitilafu? Njoo upate msaada. 

Tutamaliza shida ya kompyuta yako!

 

Ufungaji wa umeme

Je, unahitaji marekebisho ya ufungaji wa umeme nyumbani, ofisini au katika karakana yako? Wasiliana nasi. 

Karibu tutatue shida yako!

Our Trainees are sent  to the field work to get more practical Training in terms of ICT and Electricity in different Location around Tanzania

Electrical installation students in the field works.

Huduma ya kompyuta (TEHAMA)

Huduma za software

Je,unahitaji software mpya kwenye kompyuta yako? Tutakushauri na kukuwekea software sahihi.

Ushauri kuhusu kompyuta

Ushauri kuhusu kompyuta Unahitaji kompyuta mpya na hujui ipi ununue?
Tutakusaidia kujua ipi ya kununua kulingana na mahitaji yako.

Msaada wa kitaalamu

Unapata changamoto kwenye kompyuta yako?
Karibu tukusaidie!

Ubunifu wa Nyaraka
Je, unataka kuandika barua au kuandaa nyaraka nyingine?
Wasiliana nasi, fika kwetu kisha tukutengenezee upendavyo!

Ripoti, Kazi za kihasibu, Takwimu

Je, unataka kuandaa ripoti aua taarifa za kihasibu kwenye excell-sheet? Karibu tukufanyie kazi hiyo kitaalamu!

Huduma za umeme

Ufungaji wa umeme nyumbani

Tutakuwekea mfumo wa umeme nyumbani kwako ndani ya wilaya ya Muleba kwa bei nafuu.
We will come along and do the work for a resonable price!

Kuunganisha umeme kwenye mashine kubwa

Je, wataka mashine yako iunganishwe kwenye mfumo wa umeme?
Sisi tupo tayari kukuunganishia mashine yako kwa usalama kabisa!

swSwahili